Hii ni kozi ya bure inayokufundisha msingi wa usanifu na usimamizi wa mitandao kwa kutumia programu maarufu ya Cisco Packet Tracer. Imeundwa mahsusi kwa wanaoanza, wanafunzi wa IT, na yeyote anayetaka kuingia kwenye dunia ya mitandao kwa lugha rahisi ya Kiswahili.
Katika kozi hii utajifunza mambo muhimu kama:
✅ Jinsi ya kudownload na kuinstall Cisco Packet Tracer kwenye kompyuta yako
✅ Utangulizi na muonekano wa programu
✅ Kuunda LAN (Local Area Network) rahisi
✅ Kuweka IP address kwa mikono (manual)
✅ Kuunganisha vifaa vya mtandao kama switch, router, na PC
✅ Kupima na kuthibitisha uunganisho wa mtandao kwa kutumia amri kama ping
Kozi hii ni chaguo bora kwa wanafunzi wa vyuo, walimu wa IT, wanaoanza kujifunza CCNA, au yeyote anayependa kujifunza mitandao kwa lugha ya Kiswahili.
🔹 Kompyuta inayoweza kuendesha Cisco Packet Tracer (Windows, Linux au macOS)
🔹 Basic computer literacy (kujua kutumia kompyuta)
🔹 Intaneti ya kuweza kudownload programu
🔹 Hakuna maarifa ya awali ya mitandao yanayohitajika
🔸 Wanafunzi wa IT na Computer Science
🔸 Walimu wa masomo ya TEHAMA/ICT
🔸 Wanafunzi wanaojiandaa na mitihani ya CCNA
🔸 Wanaoanza kujifunza Computer Networking
🔸 Yeyote anayependa kujifunza mitandao kwa lugha ya Kiswahili
🔸 Wanafunzi wa shule za sekondari au vyuo vya ufundi