Kozi hii ya Live Class ya Website Development bila Coding (WordPress) imeandaliwa mahsusi kwa wale wote wanaotaka kujifunza kutengeneza website za kisasa, salama na zenye muonekano wa kitaalamu, bila kuhitaji ujuzi wowote wa programming kama HTML, CSS au PHP.
Kupitia darasa la moja kwa moja (Live Class) litakalofanyika tarehe 01/02/2026, mshiriki atafundishwa kwa vitendo (practical) jinsi ya:
Kuandaa mazingira ya kazi (local server) kwa ajili ya website
Kuinstall na kusetup WordPress kwa usahihi
Kutengeneza website kuanzia mwanzo hadi mwisho
Kuchagua na kubadilisha muonekano wa website (themes)
Kutumia plugins muhimu kuongeza uwezo wa website
Kutengeneza kurasa muhimu kama Home, About, Services, Contact
Kuifanya website iwe responsive (ifanye kazi vizuri kwenye simu na computer)
Kuweka misingi ya SEO (Search Engine Optimization) ili website ionekane kwenye Google
Kuandaa website iwe tayari kwa matumizi ya biashara, taasisi au personal brand
Kozi hii itafundishwa kwa lugha ya Kiswahili, kwa mtiririko unaoeleweka kirahisi, ikizingatia mahitaji ya soko la Afrika Mashariki na Tanzania kwa ujumla.
Baada ya darasa hili, mshiriki atakuwa na uwezo wa kujitengenezea website mwenyewe, au hata kuanza kutoa huduma za kutengeneza website kwa WordPress kwa wateja.
📅 Tarehe ya Live Class: 01 Februari 2026
🎓 Aina ya Kozi: Live Online Class
🌍 Platform: somataaluma.com
Ili mshiriki aweze kufuatilia na kushiriki kikamilifu katika kozi hii, anatakiwa awe na yafuatayo:
💻 Laptop au Desktop Computer (inashauriwa zaidi kuliko simu)
🌐 Internet connection ya uhakika kwa ajili ya Live Class
📧 Email address inayofanya kazi kwa mawasiliano na upatikanaji wa kozi
🧠 Uelewa wa msingi wa matumizi ya computer (basic computer skills)
🖥️ XAMPP (Local Server) tayari imesha-installiwa kwenye computer
Apache & MySQL ziwe zinafanya kazi
Mtumiaji awe tayari kutumia localhost
📂 Uwezo wa kufungua na kusimamia mafaili kwenye computer (folders & files)
❌ Hakuna ujuzi wa coding unaohitajika (HTML, CSS, PHP sio lazima)
🎧 (Hiari) Headphones au earphones kwa usikivu mzuri wakati wa Live Class
⚠️ Muhimu:
Kozi hii haitajumuisha mafunzo ya kuinstall XAMPP, hivyo mshiriki anatakiwa awe tayari amesha-install XAMPP kabla ya tarehe ya darasa ili kuweza kufuatilia mafunzo kwa vitendo bila changamoto.
Wanaoanza kabisa (Beginners) bila ujuzi wa coding
Wafanyabiashara wanaotaka website ya biashara zao
Wanafunzi wa vyuo na taasisi za elimu
Entrepreneurs & content creators
Watu wanaotaka kujiajiri kwa kutengeneza website kwa WordPress
Walimu, taasisi na NGOs wanaotaka website zao binafsi