Python Programming Essentials ni kozi ya msingi iliyoundwa kwa wanafunzi wanaotaka kuanza kujifunza programu tangu mwanzoni. Python ni lugha maarufu duniani inayotumiwa kwenye Data Science, Web Development, Machine Learning, Automation, Cybersecurity na hata A.I.
Katika kozi hii, utajifunza hatua kwa hatua namna ya kuandika programu zako mwenyewe, kuelewa misingi ya Python, kufanya debugging, kushughulikia makosa, kutumia mifumo ya kudhibiti mtiririko (control flow), kujenga kazi (functions), kutumia modules, kufanya file handling, hadi msingi wa Object-Oriented Programming (OOP).
Kozi hii imetengenezwa kwa mtindo wa mafunzo ya vitendo (practical learning) ikiwa na:
Video fupi, wazi na rahisi kufuata
Mafunzo ya mifano halisi
Mazoezi kwa kila moduli
Maswali ya kujipima (Quiz)
Mradi wa mwisho (Project)
Mwongozo wa kudownload Cheti
Kozi hii ni bora kwa wanafunzi, wafanyakazi, waalimu, freelancers, na yeyote anayetaka kujenga uwezo wa kuandika programu kutoka sifuri.
Kompyuta (Windows, Mac au Linux)
Intaneti ya kawaida
Code Editor
Msingi wa English si lazima, kozi yote ni Kiswahili
Utayari wa kujifunza
Wanafunzi wa IT, CS, BIT, BCs, BSc, CCT, DIT, DCS, BITA, DITA, etc
Wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu
Freelancers wanaotaka kuingia kwenye web development, automation na data
Wafanyakazi wa ofisi wanaotaka kuongeza ujuzi wa kiufundi
Wanafunzi wa vyuo vya kati (VETA, Colleges)
Kila mtu anayependa kujifunza programu kutoka mwanzo
Wanaotaka kubadilisha taaluma (career switch)