Karibu kwenye course ya “Hacking Lab Setup” kutoka Somataaluma! Hapa utajifunza hatua kwa hatua jinsi ya kuandaa maabara ya hacking kwa ajili ya majaribio salama na halali katika mazingira yako ya kompyuta ya nyumbani (local environment). Video hizi zipo kwa lugha ya Kiswahili, na zinaelezea jinsi ya kutumia Kali Linux, VirtualBox, na zana nyingine muhimu kwa ajili ya ethical hacking, cybersecurity, na penetration testing. • Jifunze kwa usalama. • Hakikisha mazoezi yako hayakiuki sheria.
VirtualBox ni programu ya virtualization inayokuwezesha kuendesha mfumo mwingine wa uendeshaji ndani ya Windows yako. Katika video hii ya Somataaluma, utajifunza install VirtualBox on Windows hatua kwa hatua ili uweze kuunda hacking lab salama na halali kwa majaribio ya penetration testing, ethical hacking, na cybersecurity nyumbani kwako.
Metasploitable ni virtual machine iliyotengenezwa kuwa na udhaifu mzito ili ujifunze namna mbali mbali za kuhack ikiwemo kuhack database, web applications, na server-side attacks kwa usalama katika maabara yako (hacking lab). Katika lesson hii, utajifunza step by step guide ya jinsi ya kuinstall Metasploitable on VirtualBox
Windows ni mfumo wa uendeshaji (Operating System) uliotengenezwa na Microsoft, unaotumika na mamia ya mamilioni ya kompyuta duniani kote. Unajulikana kwa usanifu rahisi, uwezo wa kuendana na programu nyingi, na usalama unaoendelea kuboreshwa. Kwa kutumia Windows, unaweza kuendesha programu za biashara, michezo, na zana za kitaalamu kwa urahisi.
Katika lesson hii, utajifunza step by step guide jinsi ya kuinstall Windows on VirtualBox ili kuunda virtual machine (VM) ya Windows kama “victim” kwa majaribio yako salama ya penetration testing, ethical hacking, na cybersecurity katika mazingira yako ya nyumbani.